Zenj FM

ZEC yawataka wasimamizi kuzingatia haki, usawa kwa wapiga kura

16 August 2025, 8:48 pm

Kamishina wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Awadhi Ali Saidi, akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo.

Na Mary Julius.

Kamishina wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Awadhi Ali Saidi, amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa majimbo kuhakikisha kila mwenye haki ya kupiga kura anatekeleza haki hiyo bila kuwepo vikwazo.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Jaji Mstaafu Mheshimiwa Hamid Mahmoud uliopo katika Afisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ,Kamishina Awadhi amewataka washiriki kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya haki, usawa na kutokuwa na upendeleo.

Amewataka kutoa huduma bora kwa wananchi watakaofika vituoni na kutumia lugha yenye staha na heshima.

Aidha,  amewakumbusha kuwa nafasi yao ni ya kipekee kwani wao ndio kiunganishi kati ya Tume na wananchi, hivyo ni wajibu wao kutenda haki na kuhakikisha kila mwenye sifa ya kupiga kura anapiga kura.

Sauti ya Kamishina Awadhi.

Akitoa muktasari wa mafunzo hayo, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini B, Mariamu Majid Suleiman, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha watendaji kuelewa vizuri taratibu na miongozo ya uchaguzi pamoja na kuwajengea uwezo wa kushughulikia changamoto za kiutendaji wakati wa uchaguzi.

Sauti ya Msimamizi Msaidizi wa  Uchaguzi wilaya ya Kaskazini B Mariamu Majid Sueiman

Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kuyatumia maarifa hayo kwa vitendo ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, haki na wenye amani.

Washiriki.