Zenj FM

Mgombea mwenza ADA-TADEA: Uteuzi wa Dk. Samia ni kudra ya Mungu

15 August 2025, 5:38 pm

Mgombea mweza nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADA Tadea, Ali Makame Issa akizungumza katika hafla ya kusaini fomu ya wadhamini waliojitokeza kumdhamini mgombea wa urais kupitia chama cha ADA TADEA.

Na Mwandishi watu

Mgombea mweza nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADA Tadea, Ali Makame Issa,amesema Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tike ya chama cha mapinduzi kunatokana na kudura za mwenyezimungu na sio matakwa ya binadamu.

Ameyasema hayo katika hafla ya kusaini fomu ya wadhamini waliojitokeza kumdhamini mgombea wa urais kupitia chama cha ADA TADEA katika mkutano uliofanyika katika ofisi za chama hicho Kisauni Zanzibar.

Sauti ya Mgombea mweza nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADA Tadea,

Aidha amesema aliyekuwa balozi wa Cuba Humphire Polepole anapaswa kuchukuliwa hatua za kinizamu na chama chakek utokana na kuvunja miko na maadili pamoja na kutoa kauli ambazo zinaweza kuzorotesha misingi ya muungano ya Tanganyika na Zanzibar.

Sauti ya Mgombea mweza nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADA Tadea,

Makame amesema Rais Dk Samia amefanya kazi kubwa katika kipindi cha mpito cha uongozi wake ikiwemo kurejesha heshima ya uhusiano wa kimataifa, uhuru wa vyombo vya habari,misingi ya demokrasia ikiwemo kurejesha mikutano ya hadhara ya vya siasa na mijadala ya bunge kuripotiwa moja kwa moja na vyombo vya habari na wananfunzi wa vyuo vikuu kulipwa pesa ao za mikopo kwa wakati.

Amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu viongozi wa vyama vya siasa wanapaswa kujiepusha na lugha za uchochezi au kukashifiana ambazo zinamadhara makubwa katika misingi ya demokrasia na umoja wa kitaifa.

Sauti ya Mgombea mweza nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADA Tadea,

Aidha amewataka wanawake Tanzania bara na Zanzibar kujitokeza na kusimama imara kumtetea mwanamke wezao rais dk samia dhidi ya watu wanaojitokeza hadharani wakimbeza licha ya kuonesha uwezo mkubwa wa kuliongoza taifa na kupotosha mchakato wa kuwapata wagombea wa urais wa muungano na Zanzibar kupitia CCM.

Sauti ya Mgombea mweza nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADA Tadea,

Aliyekuwa balozi wa Cuba Humphire Polepole ameibua mjadala mkubwa kwa wanaharakati na wanasiasa tangu kudai wagombea wa urais wam uungnao na Zanzibar kupitia CCM wamechaguliwa kinyume na katibana kanuni jambo ambalo limesababisha baadhi ya wanachama wa ccm kumtaka polepole afukuzwe uwanachama kutokana na kuvunja miko na maadili ya chama hicho.