Zenj FM

ZEC yasisitiza kura ya mapema Oktoba 2025

13 August 2025, 4:52 pm

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji. Aziza Suweid akifungua mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo Zanzibar.

Na Ivan Mapunda.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC imewahakikishia wadau uchaguzi na wananchi kuwa itaendesha uchaguzi huru na wa haki huku ikisistiza kuwa kura ya mapema itakuwepo kama ilivyoanishwa na sheria ya uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji. Aziza Suweid ametoa ahadi hiyo wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo Zanzibar.
Amesema kufanikisha ufanisi wa kazi za tume ni vyema kwa wasimamizi hao kuzingatia sheria ,kanuni ,sera na taratibu zilizopo ili kuleta ufanisi katika utekezaji wa kazi za tume hiyo.
Aidha amesema dhamira ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ni kuhakikisha inafanya uchaguzi wa haki ,huru wakuaminika na unakubalika katika pande zote .

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji. Aziza Suweid.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar Thabit Faina amesisitiza kuwa kura ya mapema itaendelea kuwepo katika uchaguzi mkuu wa oktoba 2025 kama ilivyoanishwa katika sheria ya uchaguzi ya namba 4 ya mwaka 2018.

Sauti ya Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar Thabit Faina.