Zenj FM

“Kauli za Polepole zinalenga kudhoofisha umoja wa kitaifa, muungano”

24 July 2025, 2:54 pm

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Utawala Bora Zanzibar Ali Makame Issa.

Na Mwandishi wetu.

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Utawala Bora Zanzibar Ali Makame Issa amesema kauli za aliyekuwa Balozi wa Cuba Humphrey Polepole zina madhara makubwa katika kulinda misingi ya umoja wa Kitaifa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Makame amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu madai ya Polepole kuwa wagombea urais wa ccm wameteuliwa kinyume na Katiba na kanuzi za chama cha Mapinduzi kabla y a kufanyika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Sauti ya Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Utawala Bora Zanzibar Ali Makame Issa

Amesema suala la kuwepo makundi wakati wa kutafuta wagombea ni jambo la kawaida lakini chama kinapofanya maamuzi wanachama wanapaswa kuheshimu na kuwa kitu kimoja tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Makame amesema kama Kuna kikundi kina muunga mkono polepole wanapaswa
wajitokeze ili wananchi wapate kuwafahamu badala ya kupinga maamuzi ya chama kificho.

Amesema Rais Dk Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ikiwemo kuendeleza miradi yote ambayo iliachwa baada ya Rais Dk John Pombe kufariki na kesho anazindua Treni ya kubeba mizingo ya mwendo kasi.

Makame amesema Zanzibar ndani ya Muungano muda mrefu haikutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania licha ya kujitokeza kugombea lakini hakuna mzanzibari ambae amewahi kujitokeza na kupinga maamuzi baada ya Chama kuteua mgombea.

Awali akizungumza na waandishi kupitia mtandao wa Jamii Balozi polepole amesema mchakato wa kuwapata wagombea wa urais wa ccm umevunja katiba na Kanuni na unapaswa kurudiwa kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.