Zenj FM

ADC yatoa ahadi ya elimu bure hadi vyuo vikuu

21 July 2025, 5:29 pm

Mlezi wa ADC ambaye ndiye mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho Hamad Rashid Mohd akizungumza na wananchi wa jimbo la Mtambile huko katika kijiji cha Chole Wilaya ya Mkoani Pemba.

Na Is haka Mohammed.

Chama cha Allience for Democtatic Change (ADC) kimesema kikipata ridhaa ya kuongoza Zanzibar kitafanya mageuzi katika sekta ya Elimu kwa kutoa elimu bure kwa watoto wa Skuli za Maandalizi hadi ngazi ya vyuo Vikuu.
Akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Mtambile huko katika kijiji cha Chole Wilaya ya Mkoani Pemba, Mlezi wa ADC ambaye ndiye mtarajiwa wa ugombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho Hamad Rashid Mohd amesema mfumo wa sasa wa elimu haotoi fursa kwa watoto wote kunufaika na elimu bure ambayo ndio malengo ya mapinduzi.

Aidha Mohd amesema Chama Chake kikipata Ridhaa ya kuiongoza Zanzibar Kitajenga kiwanda cha Kutengeneza Komputa na Vishikwambi ili kuwezesha wanafunzi kupata urahisi wa kusoma kwa njia ya teknolojia.

Sauti ya Hamad Rashid Mohd.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Mwalim Hamad Aziz umewaomba wananchi kukiunga Mkono chama hicho na viongozi wake ambao wana historia kubwa katika siasa za Zanzibar na Tanzania.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Mwalim Hamad Aziz.

Kwa upande wake Mratibu wa Kampeni wa Chama cha ADC Mahomoud Rashid Mohamed na Kamishna wa Chama hicho Kanda ya Pemba Mariam Muhene wamesema.

Sauti ya Mratibu wa Kampeni wa Chama cha ADC Mahomoud Rashid Mohamed.