Zenj FM

Ada Tadea yasema maendeleo yanayoonekana leo ni matunda ya utulivu

14 July 2025, 6:17 pm

Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Ali Makame Issa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kikwajuni Zanzibar.

Na Mwandishi wetu.

Chama cha Ada Tadea kimesema viongozi wa dini,wanaharakati na wanasiasa wanapaswa kudumisha amani na umoja wa kitaifa hasa kwa kuzingatia kuwa Zanzibar ni nchi ya visiwa katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Ali Makame Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari kikwajuni Zanzibar, kuhusu tathmini ya miaka mitano ya uongozi wa rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi na changamoto zinazohitaji kupatiwa ufumbuzi.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Ali Makame Issa.

Amesema kuimarika kwa amani ni ndio siri ya mafanikio ya miradi mingi kuweza kutekelezwa Zanzibar ikiwemo ujenzi wa skuli,hospitali,barabara,masoko na kuongezeka kwa uwekezaji.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Ali Makame Issa.

Aidha amesema,wafanyabiashara wazalendo wameanza kujitokeza na kuazisha miradi mikubwa ya maendeleo ambayo itasaidia kuongeza ajira na mapato ya serikali.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Ali Makame Issa.

Kuhusu hali ya uchumi amesema zipo changamoto lakini hali za maisha za wananchi zinaendelea kuimarika tofauti na miaka ya nyuma ambapo tatizo la njaa lilikuwa kubwa.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Ali Makame Issa.

Uchaguzi mkuu wa zanzibar unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na vyama vya siasa vinaendelea na mchakato wa kutafuta wagombea ambao watapeperusha bendera katika uchaguzi huo.