Zenj FM

Mafunzo ya uongozi, tabianchi yawapa ari mpya wanawake Pemba

14 July 2025, 5:29 pm

Mkuu wa Habari na Mawasiliano TAMWA Zanzibar Sophia Ngalapi, akizungumza wakati wa mkutano wa siku mbili wa wakulima kujadili masuala mbalimbali ya mradi wa kuwawesha wanawake katika uongozi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Na Is-haka Mohammed.

Viongozi wa wakulima wanawake katika kilimo Msitu na Mikoko Pemba (TOT) wametakiwa kuvitumia vyombo vya habari kueleza kazi wanazoendelea nazo ikiwemo mafanikio na Changamoto wanazokumbana nazo katika harakati zao za kilimo hicho.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Habari na Mawasiliano Tamwa Zanzibar Sophia Ngalapi wakati wa mkutano wa Wakulima hao katika mkutano wa siku mbili juu ya kujadili masuala mbali mbali ya mradi wa Kuwawesha Wanawake katika Uongozi na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi uliofanyika katika Ofisi za Tamwa Mkanjuni ChakeChake Pemba.
Amesema Wakulima wa kilimo msitu na wanawake hawana budi kueleza shughuli zao kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ili kuweza kufahamika katika maeneo mengi zaidi.

Sauti ya Mkuu wa Habari na Mawasiliano Tamwa Zanzibar Sophia Ngalapi.

Nao Baadhi ya wakulima waliopo katika mradi wa ZANADAPT Pemba wamesema kuwa kilimo msitu kimeonekana kuwa mkombozi kwa mwanamke, hata hivyo wamedai kuwepo na changamoto ambazo zimekuwa ni kikwanzo katika kuendeleza kilimo hicho.

Sauti ya Baadhi ya wakulima.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanalenga kuwakumbusha wakulima viongozi katika mradi wa Kilimo msitu Pemba, juu ya kumnyajua mwanamke kiuongozi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, unaoendeshwa na Tamwa Zanzibar, Jumuiya ya Hifadhi ya Misitu ya Jamii Pemba (CFP) na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifadhi ya Misitu (CFI)kwa Ufadhili wa Serikali ya Canada.