Zenj FM
Zenj FM
10 July 2025, 4:31 pm

Na Is-haka Mohammed
CHAMA cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) kimesema dhamira yake bado ni kushika dola na kuondosha changamoto ambazo bado zinawakabili wananchi ikiwemo wanafunzi kukaa madahalia bila ya kuchangia chochote.
Kauli hiyo ya CHAUMA imetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Hashim Ringwe alipokuwa akiwahubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale Chake Chake Pemba.
Amesema chama hicho ndicho kitachoweza kuleta ukombozi wa kweli kwa wananchi na kuwaondoshea hali ya umasikini.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Salim Mwalim amesema kuwa chama chao kimekusudia kushirikiana na vyama vyengine vye mrengo wa kufanana kimtazamo wa kimageuzi ili kupata ushindi, ambapo ni hatua ya kumuenzi Muasisi wa Mageuzi Tanzania na Zanzibar Marehema Maalim Seif Shariff Hamad.
Wakito salamu katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Vijana wa CHAUMA Massoud Mambo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Kusini Pemba Mariam Saleh Juma wamewashijihisha vijana na wanawake kuwa mstari wa mbele kugombea nafasi za uongozi.