Zenj FM

Zanzibar kuadhimisha siku ya ushirika duniani Kizimkazi

3 July 2025, 11:24 am

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Shariff Ali Shariff,akizungumza na waandishi wa habari, Picha na Mary Julius.

Na Mary Julius.

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Shariff Ali Shariff, amesema maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika Duniani kwa mwaka huu yatafanyika kitaifa huko Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, siku ya Jumamosi, tarehe 5 Julai.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Shariff katika ukumbu wa ofisi yake mwanakwerekwe amesema maadhimisho hayo ni jukwaa muhimu kwa wanachama wa vyama vya ushirika na wadau mbalimbali kukutana, kujifunza na kubadilishana uzoefu.
Amesema ushirika Zanzibar una historia ndefu tangu miaka ya 1950, na kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kuimarisha sekta hiyo ambapo hadi sasa vyama vya ushirika vilivyosajiliwa vimefikia zaidi ya 7,700.
Aidha, amewataka wananchi na wanachama wa vyama hivyo kuhudhuria kwa wingi katika kilele cha maadhimisho hayo.

Sauti ya Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Shariff Ali Shariff.

Siku ya Kimataifa ya Ushirika Duniani huadhimishwa rasmi kila ifikapo Jumamosi ya kwanza ya mwezi Julai kila mwaka na kauli mbiu mwaka huu ni “Ushirika Hujenga Ulimwengu Bora”, ikisisitiza mchango wa ushirika katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.