Zenj FM
Zenj FM
18 June 2025, 7:04 pm

Na Mwandishi wetu.
Walimu waskuli za Maandalizi na Msingi wametakiwa kuyatumia mafunzo wanayopatiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwalengo la kuwawezesha wanafunzi kuweza kusoma,kuandika na kuhesabu.
Mkuu wa Ukaguzi wa Elimu Mkoa wa Kusini Unguja Zainab Abeid Juma ameyasema hayo katika Bonanza la Mtoto wa Afrika Hafla iliyofanyika katika Skuli ya Kibele Wilaya ya Kati Unguja .
Amesema kazi Kuu ya Afisi ya Ukaguzi wa Elimu Zanzibar ni kuwasimamia walimu kuweza kufahamu namna ya kuutekeleza mtaala ambao unamjenga mtoto katika maarifa, ujuzi na muelekeo.
Kwa upande wake Afisa Taaluma Maandalizi na msingi wilaya ya kati Mlenge Haji Mlenge amewaomba walimu kuwa na mashirikiano na wazazi ili kuhakikisha wanafunzi hao wanaweza kusoma,kuandika na kuhesabu.
Nao baadhi ya Walimu kutoka skuli mbalimbali za Wilaya hiyo wamewaomba Walimu wenzao kufanya kazi kwa mashirikiano ili kufikia malengo waliojiekea.
Jumla ya Skuli 50 za Maandalizi za Wilaya ya Kati zimeshiriki katika Bonanza hilo la Mtoto wa Afirika ambalo limeambatana na sherehe mbalimbali za Michezo.