Zenj FM
Zenj FM
12 June 2025, 5:01 pm

Na Mary Julius.
Chama Cha Wanunuzi vitu chakavu Zanzibar wamesema kumekuwa na ufanisi mkubwa wa huduma za minada tangu kuazishwa Ofisi ya Msajili wa Hazina na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.
Hayo yamesemwa na msemaji wa chama hicho, Ali Makame Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari kikwajuni mjini Zanzibar, kuhusu minada ya serikali kufanyika kwa uwazi na mabadiliko ya utendaji yanayojitokeza tangu kuazishwa kwa ofisi hiyo.
Hata hivyo amesema kwamba Rais wa Zanzibar anapaswa kumlinda msajili wa hazina kwa mabadiliko anayoendelea kuyafanya na kuweza kukusanya mapato ya serikali kwa asilimia 76 kinyume na siku za nyuma katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Aidha amesema minada ya serikali hivi sasa inafanyika kwa uwazi ikiwemo kutangazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,na vitu kuuzwa kwa wakati muwafaka wakati zamani vinakaa hadi kuharibika.
Amesema haikuwa muwafaka baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kushtumu mabadiliko ya kiutendaji yanayoendelea kufanyika ndani ya ofisi ya mfuko wa hazina bila ya kuwapa nafasi ya kuwasikilizai kiwemo wadau wa minada inayofanywa na serikali.
Naye Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Ali Omar Faki amesema mafanikio yanayoendelea kujitokeza tangu kuazishwa kwa ofisi hiyo kumeweza kutoa ajira zaidi ya 200 kupitia wauza vyuma chakavu Zanzibar.
Akiwasilisha bajeti ya waziri wa nchi ofisi ya rais, fedha na mipango waziri wa wizara hiyo Dk Saada Mkuya salamu amesema, kuna baadhi ya majengo ya serikali hali yake sio nzuri na yanahitaji ukarabati na ofisi ya hazina imeanza mchakato wa kuyatengeza kwa kutumia wakandarasi wa ndani.