Zenj FM

Mtoto wa mwaka mmoja na nusu afariki kwa kudumbukia kisimani Jumbi

5 June 2025, 4:40 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Shillah.

Na Mary Julius

Mtoto Kelvin Maxmilian mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu amefariki dunia kwa kudumbukia katika kisima kilichopo nyumbani kwao Jumbi wilaya ya Kati mkoa wa kusini unguja.
Akizungumza na Zenj Fm Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Daniel Shillah amethibitisha kutokea kwa kifo hicho amesema tukio hilo limetokea tarehe 4 mwezi huu wa sita amesema mtoto huyo alikuwa akicheza karibu na nyumba yao na karibu na eneo hilo kulikuwa na kisima cha maji ambalo mfuniko wake ni mbovu hivyo katika kutambaa mtoto huyo alidumbukia katika kisima hicho.
Kamanda Shillah amewataka wazazi na walezi kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari dhidi ya vitu hatarishi vilivyopo kwenye makazi yao, hasa visima vya maji vilivyo wazi ambavyo vinaweza kusababisha majanga kwa watoto.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Shillah.

Aidha Kamanda ameitaka jamii kuchukua hatua madhubuti katika vitu hatarishi ambavyo vinaweza kuleta madhara katika jamii kwa kufunika visima kwa kutumia vifuniko imara, kuweka uzio na kufunika mashimo yasiyotumika pamoja na mienendo ya watoto wao, hasa nyakati ambazo wanakuwa wakicheza nje ya nyumba.