Zenj FM
Zenj FM
4 June 2025, 5:24 pm

Na Mary Julius.
Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis amesema Wizara kwa kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (ZARI) imeweza kutoa taaluma za udhibiti kwa wataalamu na wakulima ambapo jumla ya wataalamu 18 na wakulima 240 walipatiwa mafunzo ya udhibiti wa wadudu waharibifu.
Waziri ameyasema hayo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo Chukwani, nje kidogo ya mji wa Zanzibar,wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la wawi Bakari Hamad Bakari aliyetaka kujua mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi yamesaidia vip kukabiliana na uzaaji na uvamizi wa wadudu waharibifu wa mazao na kuongeza uzalishaji nchini.
Waziri amesema mbegu mpya zinazostahamili maradhi na mashambulizi ya wadudu zimezalishwa, mitego na dawa za kudhibit inzi waharibifu zimegaiwa kwa wa kulima 1,000 pamoja na tafiti za kukabiliana na chumvi katika udongo kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari.
waziri amesema Wizara ina imani kubwa kuwa mbinu hizi ni sahihi na madhubuti katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza uzalishaji.