Zenj FM

Wananchi wahimizwa kuchukua tahadhari dhidi ya majanga Wilaya ya Kati

24 May 2025, 9:18 pm

Afisa wa kukabiliana na Maafa Wilaya ya Kati  Ali  Haji Khamis akikabidhi  Vifaa vya Ujenzi Wananchi waliokumbwa na Maafa ya kuunguliwa na Moto pamoja na Upepo katika Wilaya hiyo.

Wilaya ya Kati.

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari ya Majanga mbalimbali yanayotokezea  katika Jamii ikiwemo Majanga ya kuunguliwa na Moto na Upepo mkali.

Afisa wa kukabiliana na Maafa Wilaya ya Kati  Ali  Haji Khamis ameyasema hayo wakati akiwakabidhi  Vifaa vya Ujenzi Wananchi waliokumbwa na Maafa ya kuunguliwa na Moto pamoja na Upepo katika Wilaya hiyo.

Amesema Wilaya ya Kati nimiongoni mwa sehemu inayotokea Majanga hayo mara kwa mara hivyo Wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari pindi wanapojenga Nyumba zao.

Sauti ya afisa wa kukabiliana na Maafa Wilaya ya Kati  Ali  Haji Khamis.

Kwa upande wao Diwani wa Wadi ya Ubago Ussi Ali Mtumwa na Diwani wa Wadi ya kiboje Haji Mzee Ali wameeleza kuwa miongoni mwamajukumu yao nikushirikiana na Wananchi kwa hali na mali pindi yanapotokezea Majanga kama hayo katika Wadi zao.

Sauti za Madiwani.

Nao Wananchi waliokabidhiwa Vifaa hivyo wameipongeza Serikali ya Wilaya kwa kuwaona kwa jicho la huruma na kuweza kuwapatia msaada huo.

Sauti za wananchi.

Vifaa walivyokabidhiwa ni Mabati pisi 20 kwa awamu ya mwanzo kwa kila Muathirika amekabidhiwa bati Kumi 10.