Zenj FM

Mashirikiano ndiyo nguzo ya kufanikisha malengo ya serikali

23 May 2025, 7:18 pm

Mkurugenzi wa zamani wa Baraza la Mji Kati Salum Muhammed Abubakar kwa pamoja na Mkurugenzi mteule Dokta Mwanaisha Ali Said pichani wakisaini makabidhiano ya majukumu ya Ofisi katika Ukumbi wa Baraza la Mji Kati Dunga.

Wilaya ya Kati.

Kuwepo kwa mashirikiano mazuri katika Taasisi za Umma ni chachu ya kufika malengo waliojiekea katika kuwaletea maendeleo Wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Kati Cassian Gallos Nyimbo ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya Ofisi kwa mkurugenzi mpya w Baraza la mji Kati ghafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la hilo Dunga wilaya ya kati.
Amesema mashirikiano ni jambo muhimu katika kazi hivyo kunakila sababu kuhakikisha mashirikiano hayo yanaimarika.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kati Cassian Gallos Nyimbo.

Kwa upande wake Mkurugenzi mteule wa Baraza la Mji Kati Dk Mwanaisha Ali Said amesema licha ya kufanya kazi sehemu mbali mbali lakini bado anahitaji mashirikiano katika utendeji wa kazi ili kufanya kazi kwa ufanisi unaotakiwa.

Sauti ya Mkurugenzi mteule wa Baraza la Mji Kati Dk Mwanaisha Ali Said.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mstaafu Salum Mohammed Abubakar amemuomba Mkurugenzi huyo kufanya kazi kwa mashirikiano na Watendaji wa Baraza hilo ili kuongeza kasi ya Usafi na ukusanyaji wa Mapato katika Baraza.

Akishuhudiana makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Baraza hilo Said Hassan Shaaban pamoja na Madiwani na Watendaji wa Baraza la Mji Kati amesema watahakikisha wanashirikiana kwapomoja katika utendaji wa majukumu yao ili lengo la serikali liweze kufikiwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa Baraza hilo Said Hassan Shaaban.

Makabidhiano hayo yamefanyika rasmin leo tarehe 23/5/2025 katika Ukumbi wa Baraza hilo Dunga.