Zenj FM

Wafanyabiashara watakiwa kulipa kodi kwa wakati kwa maendeleo ya taifa

25 April 2025, 4:24 pm

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohd Mahmoud akizindua ofisi ya Mamlaka ya mapato Tanzania TRA.

Na Mary Julius

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohd Mahmoud amewahimiza wananchi wafanya biashara na wawekezaji kulipa umuhimu suala la kulipa Kodi kwa wakati kwa maendeleo ya Taifa
Ayoub ametoa kauli hiyo huko paje wakati akizindua ofisi ya Mamlaka ya mapato Tanzania TRA ikiwa ni shamra shamra za kuelekea katika maadhimisho ya miaka 61 ya muungano WA Tanganyika na zanzibar
Amesema hatua hiyo itasaidia nchini kutekeleza na kuimarisha Vyema miundo mbinu ya kijamii katika sekata mbali mbali ikiwemo elimi,afya,maji safi na salama nishati na Barbara
Amesema viongozi wa serekali zote mbili wana dhamira za dhati za kuwaletea maendeleo wanchi katika nyanja za kiuchumi na kijamii hivyo ni Vyema kwa wafanya biashara kuondokana na tabia ya kukwepa kulipa Kodi kwani kufanya hivyo kunaikosesha serekali mapato
Akizungumzia kuhusu suala la Muungano amesema wanchi wanapaswa kuendelea kujivunia matunda na mafanikio ya muungano huo huku wakizingatia kuendeleaza misingi ya umoja amani na upendo katika nchi.

Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Zanzibar Saleh Pandu amesema katika kipindi cha miezi tisa kutoka mwaka mpya wa fedha 2024/2025 Mamlaka hiyo imeweza kupiga hatua kubwa ya ukusanyaji wa mapato kwa kukusanyo zaidi ya bilioni mia nne ukilinganisha na mwaka wa fedha 2023 ambao ulikusanya bilioni mia tano na nane hali iliyopelekea Serikali zote mbili kupiga hatua katika sekta za kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake Meneja Mlipa Kodi Wilaya ya Kusini Issa Hamdani Juma amesema kuweko kwa ofisi za TRA katika Wilaya hio kutawaondoshea usumbufu wananchi kufuata huduma hio masafa ya mbali na kuzidi kuwasisitiza kuendelea kudai risiti za elektroniki kila wanapofanya matumizi.