Zenj FM
Zenj FM
18 April 2025, 4:29 pm

Baraza la mji Kati.
Baraza la Mji Kati wametakiwa kufuata taratibu, sheria na Kanuni zilizowekwa na Serikali pindi wanapotaka kuanzisha Viwanja vya kufurahia Watoto kwalengo la kuwa na Viwanja vilivyo bora.
Meneja Mipango kutoka ZSSF ambae pia Msimamizi wa Viwanja vya kufurahia Watoto Kariakoo Unguja Abdul Azizi Mohammed Ramia ameyasema hayo huko Ofisini kwake ZSSF Kilimani Mjini Zanzibar.
Amesema Baraza la Mji Kati watakapofuta Miongozo iliyowekwa watapata mafanikio makubwa na itapelekea kuongezeka kwa Mapato katika Baraza hilo na kufikia Malengo waliojiwekea.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Baraza la Mji Kati Rehema Khamis Hassan amesema lengo la kufika katika afisi za ZSSF ni kutaka kufahamu namna gani wanaendesha shughuli hizo pomoja na kujifunza mambo mbalimbali.
Nae Mkuu wa Divisheni ya Mapato Uchumi na Wajasiriamali wa Baraza hilo Helena John Bartholomeo ameahidi kuifanyia kazi elimu waliopatiwa kwa lengo la kurejesha haduma kwa Jamii pia kuongeza Mapato katika Baraza hilo
Mkuu wa Divisheni ya Mapato Uchumi na Wajasiriamali wa Baraza hilo Helena John. Jumla ya Maafisa watano 5 Kutoka katika Kitengo cha Mapato, Mipango na Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Baraza la Mji Kati wameshiriki katika Ziara hiyo.