Zenj FM
Zenj FM
18 April 2025, 3:19 pm

Mwenyekiti wa Umoja wa Watu wenye ulemavu Zanzibar Abdulwakili H Hafidhi (aliye kaa kati) akiwa na baadhi ya viongozi wa Umoja huo.Na Mary Julius.
Katika jitihada za kuwawezesha wanawake wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika jamii na kutambua haki zao, Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ) umeandaa mafunzo maalum yaliyojikita katika masuala ya haki za binadamu, usawa wa kijinsia na haki za watu wenye ulemavu.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa UWZ Kikwajuni, Wilaya ya Mjini, yakihusisha wanachama wa kikundi cha Wanawake Wenye Ulemavu Kusini (WUKU).
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa UWZ, Abdulwakil H. Hafidh, amesema lengo kuu ni kuwaongezea wanawake hao uelewa kuhusu nafasi yao katika jamii, pamoja na kuwapa maarifa ya kujilinda dhidi ya unyanyasaji na ubaguzi wa aina yoyote.
Aidha Mwenyekiti Abdulwakili amewaomba masheha kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za watu wenye ulemavu walioko katika shehia zao, ili kuhakikisha hakuna mtu mwenye ulemavu anayeachwa nyuma katika kupata haki na huduma muhimu.
Mwenyekiti wa Umoja wa Watu wenye ulemavu Zanzibar Abdulwakili H Hafidhi.Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo, Khairun Khalid Mambo, amesema mradi huu ulio fadhiliwa na Action on Disability and Development (ADD) umelenga kuwawezesha wanawake wenye ulemavu kiuchumi pamoja na kuwapatia mafunzo yanayohusu haki za watu wenye ulemavu.
Amesema kupitia mradi huu, washiriki watajengewa uwezo wa kujitambua, kutetea haki zao, na pia kuandaa miongozo maalum ya kuwawezesha watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali za maisha.
Aidha, Khairun amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha elimu waliyoipata wanaisambaza kwa watu wengine katika jamii ili ifike mbali zaidi na kuleta mabadiliko ya kweli kwa watu wenye ulemavu.
Mratibu wa mafunzo hayo, Khairun Khalid Mambo.
kufunzi katika mafunzo hayo Mwema Ali Ameir.Nae Mkufunzi katika mafunzo hayo Mwema Ali Ameir amesema mafunzo hayo yatawawezesha wanawake wenyenye ulemavu wilaya ya kusini kutambua haki zao wajibu wao katika shughuli zao za kila siku.
Mkufunzi katika mafunzo hayo Mwema Ali Ameir. Kwa upande wao Washiriki wa mafunzo hayo wameupongeza umoja huo kwa kutoa mafunzo hayo , wameahidi kuifikisha elimu hiyo kwa jamii kwa vitendo, ili kusaidia kuwanusuru watu wenye ulemavu dhidi ya changamoto zinazotokana na kutozitambua haki zao.
Mada mbili zimewasilishwa katika mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika kila mwezi mara moja kwa muda wa miezi sita ambazo ni kuhusu ulemavu na yapili ni mikataba ya kimataifa na haki za watu wenye ulemavu.