Zenj FM

Fursa kwa vijana kuzinduliwa kwa programu mpya ya Mobile Youth Space

11 April 2025, 4:23 pm

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab

Na Berema Suleiman Nassor

Kuzinduliwa kwa Programme ya Mobile Youth Space na Amani ni Tunu,Vijana Tuienzi itaweza kusaidia kuimarisha ushiriki wa upatikanaji wa taarifa kwa vijana.
Akizungumza na wandishi wa habari Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab amesema vijana wengi bado wanakabiliwa na changamoto ya ushiriki na ushirikishwaji katika mambo yanayowahusu na hatimae kukosa fursa na nafasi mbalimbali katika jamii ikiwemo nafasi za uongozi hivyo kupitia programme hizo zitawawezesha kuzifikia fursa mbalimbali ikiwemo ajira.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa shirika la SOS Gharib Abdalla Hamad amesema shirika hilo ni wadau wakubwa wa maendeleo ya vijana hivyo wataendelea kuunga mkono juhudi za wizara hiyo ili kuweza kufikiwa kwa maendeleo bora ya vijana hapa nchini.

Sauti ya kaimu mkurugenzi wa shirika la SOS Gharib Abdalla Hamad.