

30 March 2025, 8:46 pm
Na Mary Julius.
Jeshi la Mkoa wa kusini unguja limesema mtu mmoja, amefariki dunia kwa kupigwa na kitu butu kichwani huko Hanyengwa, wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Akizungumza na zenji fm Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Daniel Shillah amesema watu wasio fahamika wamemshambulia na kitu butu kichwani mtu huyo aliyefahamika kwa Jina la Juma Lubinza, miaka 45 msukuma mkaazi wa Cheju ambapo katika shambulio hilo lilipelekea kifo chake.
Akizungumzia chanzo cha tukio hilo kamanda Shillah amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi ulioibuka kwenye club ya pombe za kienyeji.
Aidha Kamanda amewataka wananchi kuwa waangalifu na kuepuka ulevi kupita kiasi hasa wakati wa sikukuu, na kuachana na tabia ya kujihusisha na matukio ya vurugu zinazotokana na matumizi ya pombe.