Zenj FM

Polisi Mjini Magharibi watoa wito wa amani kuelekea sikukuu ya Eid-el-Fitr

28 March 2025, 5:42 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Mchomvu.

Na Said

Kuelekea Sikukuu ya Eid-el-fitri Jeshi la Polisi mkoa wa mjini magharib llimetoa wito kwa wananchi kusherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu na isiwe chanzo cha kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwemo, wizi, uporaji, unyang’anyi, udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Mchomvu, amewaasa madereva wenye tabia ya kuendesha vyombo kwa mwendo kasi pamoja na kupiga misere (Drifting) kwenye barabara ikiwemo eneo la Michenzani, barabara ya Fumba, Fuoni, Uwanja wa ndege na maeneo mengine kuacha tabia hiyo.
Kamanda amewaomba wananchi kutotumia magari yasiyo rasmi au yasiyosajiliwa kwa ajili ya kupakia abiria kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria, pia ni kuhatarisha maisha ya dereva, abiria na watumiaji wengine wa barabara.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Mchomvu.

Kamanda Richard ametoa tahadhari kwa wamiliki wa kumbi za starehe kuhakikisha kwamba wanafuata taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo kwa kuzingatia muda wa kufunga kama ulivyoelekezwa katika vibali vyao.
Aidha, amesema katika kudhibiti ajali za barabarani, katika kipindi cha sikukuu baadhi ya barabara zitafungwa kwa muda.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Mchomvu.