

27 March 2025, 1:58 pm
Na Omar Hassan.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kubaka watoto katika matukio mawili tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Tunguu, Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Shillah amesema tukio la kwanza linamhusisha Yasin Said Self miaka 14 mkazi wa Paje ambaye anatuhumiwa kumwingilia mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, tukio ambalo limetokea Machi 15,2025 majira ya saa 07.00 mchana huko Paje Wilaya ya Kusini.
Amesema, katika tukio jingine Nyambo Suleiman Luponya miaka 18 mkazi wa Kiboje Kinooni ambaye anatuhumiwa kumwingilia mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 9 tukio lililotokea Machi 24,2025 huko Kiboje Kinooni Wilaya ya Kati.
Kamanda Shillah amesema Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani haraka kujibu tuhuma zinazowakabili.