Zenj FM

Wanawake watakiwa kulinda watoto dhidi ya udhalilishaji kwenye biashara

14 March 2025, 5:01 pm

Baadhi ya wajasirimali wakisikiliza mafunzo huko skuli ya Tumekuja wilaya ya Mjini.

Na Mary Julius.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Siti Abasi Ali, amesema mafunzo ya ujasirimali yamesaidia kuhamasisha wanawake na vijana kujikwamua kimaisha kupitia sekta ya ujasiriamali.
Ameyasema hayo katika mafunzo yaliyotolewa kwa wanawake na vijana wajasirimali, mafunzo yaliyofanyika katika skuli ya Tumekuja Mkurugenzi Siti amesema mafumzo hayo yatawasaidia wanawake na vijana kuwa na uhuru wa kifedha na kujitengenezea ajira wao wenyewe.
Mkurugenzi amesema kufanya biashara ndio njia moja wapo ya kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia,amesema mtu anapokuwa na kipato chake mwenyewe na kujitegemea, anakuwa na nguvu ya kujilinda na kujiepusha na mazingira ya kudhalilishwa au kutegemea msaada wa wengine.
Aidha Mkurugenzi ametoa wito kwa wanawake kuwa makini na kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya udhalilishaji, hasa wanapokuwa wanajishughulisha na biashara.
Kwa upande wake mjasirimali Nasma Ali Abdallah ameshukuru kwa kupewa mafunzo hayo ambayo yatakwenda kubadilisha maisha yake na jamii inayo mzunguka.
Aidha ameahidi kuwafikishia wanawake wengine elimu,nao waweze kujishughulisha na kazi zitakazowaingizia kipato ili kuepukana na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake.

Sauti ya Mjasirimali Nasma Ali Abdallah.