

27 February 2025, 5:47 pm
Na Mary Julius.
Afisa Mipango Wilaya ya Magharib b Faida Khamis Ali amesema bajeti ya mwaka 2025 2026 imezingatia mapendelezo yaliyo tolewa na Mabaraza ya watoto.
Afisa ameyasema hayo wakati Akifungua kikao cha watoto wadau wa asasi za kiraia na serikali juu ya mapendelezo ya bajeti kwa watoto,kikao kilichofanyika skuli ya tumekuja
Aidha Amesema wilaya ya Magharib b itahakikisha maslahi ya watoto yanazingatiwa katika mchakato wa kupanga bajeti, na sauti za watoto, kupitia mabaraza yao, zinapewa kipaumbele katika maendeleo ya jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Division ya Mapendelezo ya Watoto Mohammed Jabil amesema lengo la mkutano huo ni kukumbushana mapendekezo ya shughuli za bajeti zinazo gusa mabaraza ya watoto pamoja na kuimarisha, Uwajibikaji kati serikali na asasi za kiraia katika ushikishaji na kuimarisha mabaraza ya watoto.
Aidha amesema uwepo wa uhaba wa rasilimali fedha umesababisha kupunguza utekelezaji wa uimarishaji wa mabaraza hayo.
Nae Mratibu Jukwaa la Haki za Watoto ZCRF Sophia Leghela amesema lengo kubwa ni kuhakikisha watoto wanatengewa bajeti Yao katika bajeti ya taifa ili kuimarisha mabaraza yao
Aidha amesema asasi za kiraia zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha zinaisaidia serikali katika kuimarisha mabaraza ya watoto.
Wakitia michango yao washiriki katika mkutano huo wameiomba wizara ya elimu kuangalia suala Zima la adhabu maskuli ili kujenga jamii iliyo bora.