

3 February 2025, 4:31 pm
Is-haka Mohammed.
Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi UWT Zanzibar Zainab Khamis Shomari amewataka wamachama wa chama hicho Kisiwani Pemba, walio na sifa za kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kujitokeza ili kuandikishwa katika zoezi lililoanzia katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akizungumza na wana CCM katika hafla ya ufunguzi wa Maskani ya Dkt. Omar Ali Juma na Bekari ya Dkt Omar iliyopo katika kijiji cha Shimindu, jimbo la Ole Wilaya ya Chake Chake Pemba iliyojengwa na Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia UWT Mkoa wa Kusini Pemba Lela Mohamed Mussa Zainab amesema kuandikishwa ndiyo fursa itakayomwezesha mtu kupiga kura.
Naye Mwakikilishi wa Viti maalum kupitia wasomi Mkoa wa Kusini Pemba ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar amesema ujenzi wa maskani hiyo na Bekar ya kisasa ni kumuenzi aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Dr. Omar Ali Juma ambaye anatoka kijijini hapo.
Katika hafla hiyo Mwakilishi Lela amemkabidhi Makamo Mwenyekiti huyo wa UWT Zainab Khamis Somari Jumla ya Milioni 10 ili zitumike kwa wajili ya kuimarisha uendeshaji wa bekari hiyo, pikipiki ya kusambazia mikate, jezi na mipira kwa vijana wa shimindu huku wana ccm wao wakimkarimu Makamo Mwenyekiti huyo zawadi mbali mbali