Serikali ya Uingereza na Serikali ya Tanzania zaahidi kuendeleza mashirikiano
20 January 2025, 3:37 pm
Na Omar Hassan.
Serikali ya Uingereza na Serikali ya Tanzania zitaendelea kushirikiana katika kukabiliana na makosa makubwa yanayovuka mipaka ili kuzidisha hali ya usalama na ustawi wa jamii wa nchi hizo.
Akizungumza katika ziara ya Maafisa kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Mkuu wa Kitengo cha Uhalifu Mkubwa wa kupangwa na kupambana na Makosa ya Ufisadi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Felix Wood amesema Serikali ya Uingereza imelenga kuzisaidia Taasisi za Tanzania zinazoshushughulika kuzuwia makosa makubwa yanayovuka mipaka ili kuleta mafanikio katika kuzuwia makosa hayo.
Nae Naibu Mkurugezi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Zuberi Chembera amesema Kufuatia Ziara ya Maafisa Kutoka Ubalozi wa Uingereza Jeshi la Polisi limeahidiwa kiupatiwa vitendea kazi na taaluma hasa katika upelelezi wa uhalifu wa kimtandao.
Aidha ameimeishukuru Serikali ya Uingereza pamoja na Wizara ya Sheria, Katiba, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar kwa kuwa karibu na Jeshi la Polisi kwa kuwasogeza karibu na Taasisi wahisani katika Mapambano dhidi ya Uhalifu.