Zenj FM

Kashfa ya maneno  na vitendo zinavyotesa wanawake kuwania nafasi za uongozi Zanzibar

6 December 2024, 6:51 pm

Mkurugenzi wa haki za binadamu na sheria katika Chama Cha Wananchi – CUF Nadhira Ali Haji. picha na Ivan Mapunda.

Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 inaonesha Zanzibar ina watu 1,889,773 kati ya hao wanaume ni 915 ,492 na wanawake ni 974 ,281 hii ina manisha kwamba wanawake ni asilimia 51.6 ya wakaazi wote Zanzibar.

Licha ya wanawake kuwa wengi bado kumekuwa na upungufu wa wanawake kushiriki katika kushika nafasi za uongozi katika ngazi za maamuzi na nafasi za chama kutokana na vikwazo tofauti vikiwemo kashfa ya maneno na vitendo wakati wa kujitoa kuingia kwenye uchaguzi au hata kwenye kampeni.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake tanzania upande wa Zanzibar –TAMWA-Z .Katika ripoti yao june 2024 inayohusu uchambuzi wa ukatili dhidi ya wanawake katika vyama vya siasa Zanzibar imeeleza kuwa washiriki wa utafiti walirekodi visa vya ukatili wa kijinsia ni asilimia 21.88% na hakukuwa taarifa za kuripoti matukio hayo.Wanaharakati wa masuala ya kijinsia nchini wanasema vipo vikwazo vingi vinavyokwamisha jitihada za wanawake kuwa viongozi.

Sauti ya Ivan Mapunda aikisumulia katika Makala sehemu ya kwanza.
Sauti ya Ivan Mapunda aikisumulia katika Makala sehemu ya Pili na ya Mwisho.