Kikosi Cha Kuzuia Magendo KMKM Marumbi Kimefanikiwa Kukamata Watu 8 Wanaojihusisha na Uvuvi Haramu
4 December 2024, 10:01 pm
Wilaya ya Kati.
Kikosi Cha kuzuia magendo KMKM Marumbi kimefanikiwa kukamata watu 8 wanajihusiaha na uvuvi Haramu.
Akithibitisha kukamata kwa watu hao Mkuu wa Kambi hiyo Luteni Kamanda Hassan Bakari Babu amesema kikosi hicho kilifanikiwa kuwakamata watu hao wakiwa katika harakati za kuvua samaki kwa kutumia nyavu na madema ambyo ni dhana za uvuvi Haram hziruhusiwi kutumika.
Amesema kutumika kwa vifaa vya uvuvi vilivyopigwa marufuku ni Kwenda kinyume na sheria na taratibu za serekali ambapo imeonekana baadhi ya wanavijiji vitatu ikiwemo Marumbi ,chwaka na na michanvi wakviendeleza vitendo hivyo vya uvuvi haramu.
Mkuu wa wilaya ya kati Cassian Gallos Nyimbo, amesema serekali haitasita kumchikulia hatua Kali za kisheria mvunvi yoyote atakaekamatwa anajijusisha na uvuvi huo ili kuona vitendo hivyo vinamaliza kabisa katika ghuba hiyo ya chwaka na Maeneo mengine ya wilaya hiyo.
Nae Sheha wa Shehia ya Marumbi Juma Hamza Abass. na Afisa wa uvuvi wilaya ya kati Ali Mwalim Mahfoudh wamesema wataendelea kusimamia masuala ya hifadhi za bahari ili kuona wavuvi wanaondokana na masuala ya uvuvi haramu