Zenj FM

Tume huru kuchunguza ajali gari linalokimbia vikosi vya ulinzi na usalama

10 November 2024, 4:58 pm

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Zuberi Chembera Akizungumza na waandishi wa Habari huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

Na Omar Hassan

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Zuberi Chembera amesema Tume Huru imeundwa kuchunguza tukio la gari iliyokuwa ikikimbizwa na Askari wa vikosi vya ulinzi na usalama kupata ajali na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi wawili huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akizungumza na waandishi wa Habari huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar amesema matokeo ya uchunguzi wa tukio hilo yatatolewa mapema kujua kiini na sababu ya gari kukimbia na magari mengine kuwashambulia Askari pamoja na Askari kufyatua risasi.

Sauti ya Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Zuberi Chembera.

Amefahamisha kuwa katika Tukio hilo dereva wa gari aitwae Msina Sharif (29) mkaazi wa kidoti na msaidizi wake aitwae Abdalla Bakari Sheha (28) mkaazi wa kidoti walipoteza maisha na watu wengine wawili walijeruhiwa ambao ni Mohammed Issa Mohammed (10) mwanafunzi wa skuli ya msingi kidoti na hamza abdalla abasi (10) mwanafunzi wa skuli ya msingi kidoti, majeruhi hao walikuwa watembea kwa miguu wamegongwa wakati gari hilo limepoteza muelekeo na kugonga mti/Mkungu, wamelazwa Hospitali ya Kivunge kwa matibabu.

Sauti ya Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Zuberi Chembera.