Zenj FM

Bodaboda watakiwa kujisajili Zanzibar

30 August 2024, 5:48 pm

Bodaboda

Na Ester Joshua

Makamo Mwenyekiti Wa Jumuiya Ya Bodaboda Hussein Abushiri Hussein amewataka madereva wa bodaboda na bajaji kujisajili katika umoja huo  ili kupunguza uhalifu unaojitokeza  kwa madereva na abiria.

Akizungumza na Zenj FM huko  ofisi ya umoja huo huko kilimani amesema kufanya hivyo kutasaidia kupunguza uhalifu unaojitokeza kwa kiwango kikubwa na kuondoa hofu kwa wananchi ambao wanatumia usafiri huo.

    Kwa upande wake dereva wa bodaboda amesema kujisajili kumemsaidia  kuimarisha usalama ulinzi  wao pamoja na abiria wanao wabeba.