Zenj FM

Wananchi Uroa waalaani kuhamishwa makaburi

26 August 2024, 5:12 pm

Eneo la Makaburi

Eneo hilo la kuzikia kwa wananchi wa kijiji cha Uroa lilikua na mgogoro kwa muda mrefu na mahakama ikatoa uamuzi 20/08/2008 kuwa eneo hilo lisihusishwe na shunguli yoyote iwe ya ujenzi wa mazishi hadi itakapofika miaka 40 ambapo katika eneo hilo jumla ya maiti 9 zimefukuliwa kwa ajili ya kuzikwa upya katika eneo lililochaguliwa.

Na Mary Julius

Wananchi wa kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja wameelaani kitendo cha mwekezaji wa hotel ya Jaz Maluuna kufukua makaburi ya wazee wa kijiji hicho waliofariki  na kuzikwa katika eneo moja  kinyume na sheria.

Wakizungumzia kero hiyo wamesema kitendo hicho kimekuwa kikifanyika bila ya kufuata sheria kwani tayari mahakama ilishatoa hukumu ya eneo hilo kutojengwa wala kufanywa taratibu zozote za mazishi katika eneo hilo tarehe 20/08/2008 hadi itakapotimia miaka 40.

Sauti ya Wananchi Uroa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Kati Hamza Ibrahim Mahmod amesema hatua hiyo imekuja kufuatia mwekezaji kulitaka eneo hilo kwa ajili ya kuwekeza huku akisema kuwa wananchi wa kijiji hicho wameshirikiswa katika taratibu zote.

Aidha Katibu amesema serikali ya wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya Mufti ilifika katika kijiji hicho na kutoa elimu juu ya suala hilo huku akiwataka wananchi wa Uroa kutochukua sheria mikononi kwani suala hilo walishirikiswa kwa asilimia zote.

Sauti ya Katibu Tawala Wilaya ya Kati Hamza Ibrahim Mahmod.