Zenj FM

Zanzibar yaadhimisha siku ya usalama wa chakula duniani

7 June 2024, 6:24 pm

Mtaalamu WA maradhi yasiyoyakuambukiza NCDs Zuhura Saleh Amour   akichangia katika kongamano la kuadhimisha siku ya usalama wa chakula ambayo huadhimishwa Juni 7 Duniani kote,Hafla iliyofanyika Michenzani Mall Mkoa wa Mjini magharibi.

Na Mary Julius.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) inakadiriwa kuwa, kiasi ya watu 600,000,000 wanaugua kila mwaka kutokana na kula chakula kisicho salama ambapo kati ya hao watu laki nne na ishirini wanapoteza maisha.  

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanibar Dkt. Habiba Hassan Omar amewataka Wadau wa chakula nchini kuzingatia usalama wa chakula ili kulinda afya ya mtumiaji. 

Akifungua Kongamano la kuadhimisha siku ya usalama wa chakula Duniani ambapo kwa upande wa Zanzibar yamefanyika Michenzani mall Mjini Zanzibar amesema kuna madhara mengi yanayosababishwa na chakula ikiwemo Sukari na Sindikizo la damu.

Amesema jambo hilo ni tishio kwa afya za binadamu na pia linapoteza nguvu kazi ya Taifa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanibar amewataka Wanajamii kutumia mlo kamili pamoja na kufanya mazoezi ili kulinda afya na kupunguza madhara yanayotokana na chakula kisicho salama

Aidha amesema jamii inaathirika kwa kutumia vyakula visivyo salama hivyo amewataka Wakala wa Chakula na Dawa (ZFDA) kutumia maadhimisho hayo kwa kutoa elimu kwa jamii kuhusu usalama wa chakula na kulinda afya ya Mtumiaji.

Sauti ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanibar Dkt. Habiba Hassan Omar

.Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Burhan Othman Simai amesema lengo la maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kujilinda kutokana na uchafuzi wa chakula, unaopelekea matatizo mbalimbali ikiwemo magonjwa yasioamumbukiza ambayo husababisha kifo na ulemavu wa kudumu.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Burhan Othman Simai

Akitoa maelezo kuhusiana na usalama wachakula Aisha Suleiman Bundakazi kutoka wakala wa dawa na chakula ZFDA amesema chakula salama ni kile ambacho hakitamletea madhara ya kiafya mtumiaji baada ya kukitumia.

Amesema chakula salama ni chakula ambacho kimeepukana na vihatarishi vya kifizikia na kibaiolojia hivyo usalama wa chakula ni muhimu kwani chakula kisicho salama kinaweza lkuleta madhara kwa mtumiaji.

Sauti ya Aisha Suleiman Bundakazi .
Mwalimu wa Skuli ya Afya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Salim Ali Abdalla akichangia katika kongamano la kuadhimisha siku ya usalama wa chakula ambayo huadhimishwa Juni 7 Duniani kote,Hafla iliyofanyika Michenzani Mall Mkoa wa Mjini magharibi.

Akichangia katika kongamano hilo Mkufunzi wa chuo kikuu cha kilimo (SUA) Pr. Benarld Chove amesema wanaoangaliwa zaidi katika usalama wa chakula ni wakulima, wauzaji na walaji lakini kundi la wasafirishaji limesahauliwa jambo ambalo linaweza kusabaisha uchafuzi wa chakula kwa kiasi kikubwa.

Maadhimisho ya siku ya chakula Duniani hufanyika Juni 7 kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “usalama wa chakula -jiandae kwa usioyatarajia”.