Zenj FM

Mabadiliko ya tabianchi yawaibua wanahabari Pemba

20 May 2024, 4:11 pm

Waandishi wa habari kutoka Pemba Press Club wakiwa katika zoezi la upandaji wa miti ya mikoko aina ya miche huko Kambini Kichokochwe Wilaya ya Wete Pemba.

Na Is-haka Mohammed

Klabu hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wao na wanajamii kutoa elimu pamoja na kushiriki moja kwa moja kwenye harakati za kupunguza athari zaidi za mabadiliko ya tabianchi kwenye maeneo yaliyoathirika ikiwemo kupanda miti.” Amesema Mwenyekiti wa Pemba Press Club.

Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba (Pemba Press Club) na Jumuiya ya Community Forest wameshirikiana na wanakijiji cha Kambini Kichokochwe kwa ajili ya kupanda miti ya mikoko  aina michu katika eneo lililoathirika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na kupelekea athari za maji ya bahari kuingia kwenye mashamba ya mipunga na vipando vyengine.

Akizungumza katika zoezi hilo Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba Bakari Mussa Juma amesema ujumbe wa mwaka huu katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani umejikita zaidi katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi hivyo wakaona watumie sehemu katika maadhimisho yao kwa Pemba kupanda miti hiyo.

Mkurugenzi wa Community Forest Zanzibar Mbarouk Mussa amesema juhudi zaidi zinahitajika kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi zilizosababishwa na ukataji wa miti kwani kwa kisiwani Pemba inaelezwa kuna maeneo mengi yaliyoathiriwa.

Sauti ya Mkurugenzi wa Community Forest Zanzibar Mbarouk Mussa.

Katibu wa Kamati ya Uhifadhi Mazingira katika shehia ya Kambini Kichokochwe Bakar Suleiman Juma amesema wananchi wa Ukanda wa Mashariki ni waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabia nchi kutokana na kuwa karibu sana na bahari ya hindi.

Sauti ya Katibu wa Kamati ya Uhifadhi Mazingira Bakar Suleiman Juma.

Mmoja wa wananchi wa Kambini Kichokochwe Fatma Shaame Hamad ameishukuru Pemba Press Klabu na Community Forest kwa kuona umuhimu wa kushirikiana nao katika jambo hilo.

Sauti ya mwanankijiji Fatma Shaame Hamad.