DC Kusini Unguja atoa onyo wanaojichukulia sheria mkononi
14 May 2024, 3:57 pm
Na Omary Hassan
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Cassian Galos Nyimbo amesema ujenzi wa vituo vipya vya Polisi nchini uendane na matumizi ya wananchi kutafuta haki kwa misingi ya sheria na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi.
Akiweka jiwe la msingi Kituo cha Polisi Makunduchi huko Kijiji cha Makunduchi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja Nyimbo amesema ni vyema wananchi kufuata sheria katika kupata haki zao.
Amesema Wilaya ya Kusini Unguja imeanza kuwachukulia hatua na wahalifu wakiwemo wafanyabiashara ya mabaa yanayofanya biashara na kupiga mziki bila ya kuwa na leseni.
Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. Daniel Emanuel Shillah amesema kukamilika kwa ujenzi wa Jengo Jipya la Kituo hicho kilichogharimu Zaidi ya T.shs milioni 684,000,000/= kutaboresha utendaji wa Polisi katika kutoa huduma bora kwa wananchi.