Vijana Zanzibar washauriwa kuacha kuvaa mapambo
17 April 2024, 4:11 pm
Na Mary Julius.
Vijana wengi wamekuwa wakitumia urembo huo bila ya kujua unaashiria kitu gani.
Vijana wa kiume wametakiwa kuacha tabia ya kuvaa mapambo (bangili, cheni na viculture ) kwani wanakiuka mila na tamaduni za mzanzibar.
Ushauri huo umetolewa na Katibu wa Kamati ya Maadili kupitia Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZZA) Abdalla Mnubi wakati akizungumza na Zenji Fm ofisini kwake Vuga Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema uvaaji wa urembo ni haram kwa vijana na haikubaliki katika dini ya kiislam na dini ya kikiristo kwani hujifananisha na wanawake jambo ambalo Allah SW analichukia.
Aidha Katibu amesema wamekuwa wakichukua hatua za kuandaa makongamano ya mara kwa mara kuwapatia elimu hatua hiyo itasaidia vijana kukumbuka na kufuata utamaduni wao.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi wamesema hawapendelei kuwaona watoto wao wa kiume wakifanya vitendo hivyo na kupelekea kukosa hofu mbele ya Allah SW.
Nao baadhi ya vijana wamesema wanavaa mapambo kutokana na ushawishi wa vijana wenzao wakiwaona wamevaa nao huhamasika kuvaa hivyo wamewataka vijana wenzao kuacha tabia hiyo kwani sio sahihi kimaadili na kiutamaduni.