Uzalishaji taka waongezeka Zanzibar kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani
27 March 2024, 6:43 pm
Na Rahma Hassan.
Kuelekea katika kipindi cha mvua za masika wakaazii wa shehia ya mikunguni wameliomba Baraza la Manispaa Zanzibar kulitafutia ufumbuzi suala la taka zilizozagaa katika jaa la shehia yao.
Wakizungumza na zenji FM Wananchi hao Wamesema karibu wiki tatu sasa wazoaji wa taka katika shehia hiyo hawajafika kuzichukua hali ambayo inahatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo
Aidha wamesema katika eneo hilo la jaa kulikuwepo kikapu cha kuwekea taka lakini baraza hilo limekiondoa na kusababisha kuzagaa ovyo kwa taka.
Nae sheha wa shehia ya mikunguni Makame KHatib Amesema uwezo wa manispaa wa kukusanya taka umepungua hali ambayo imepelekea kuzagaa kwa taka hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar Ali Khamisi Mohd amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambalo limesababishwa na uchakavu wa vikapu vya kuwekea taka katika majaa mbalimbali Zanzibar.