Zenj FM

Wafanyabiashara Pemba wahimizwa kulipa kodi kwa hiari

13 December 2023, 3:47 pm

Afisa wa Mamlaka wa Mapato Zanzibar(ZRA) Tamima Is-Haka Mzee akikakagua matumizi ya mashine kwa mfanyibaisha mjini chake chake, ikiwa ni katika shamra shamra  za mwezi wa shukrani kwa mlipa kodi zanzibar. Picha na Is-haka Mohammed.

 

Na Is-haka Mohammed.

Mamlaka ya Mapato Zanzibar(ZRA) Pemba imezindua mwezi wa kurejesha shukrani kwa mlipa kodi kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wa Manispaa ya Chake Chake juu kulipa kodi kwa hiari na kutoa risiti za Kielekronik.

Katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa ZRA Pemba Jamal Hassan Jamal amewataka wafanyabiashara na Wananchi wa kisiwani Pemba, kulipa kodi zao kwa hiari kwa kutoa risiti za kielektronic kwani kodi hizo ndizo zinazotumiwa na serikali katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo.

Amesema katika mwezi huu wa kurejesha shukrani kwa mlipa kodi mwaka huu kwa kisiwani Pemba harakati mbali mbali zitafanyika ikiwemo kutoa misaada kwenye vituo vya kulelea mayatima, watu wasiojiweza na wale wenye mahitaji maalum.

Sauti ya Mkurugenzi wa ZRA Pemba Jamal Hassan Jamal.

Wakitoa elimu hiyo kwa wafanyanya biashara wa Manispaa ya Chake Chake Maofisa wa ZRA Pemba wametaka wafanyabiashara kuendelea kutumia mashine za kielektronik.

Sauti za Maofisa wa ZRA Pemba.

Kwa upande wao wafanyabiashara hao wamefurahishwa kufikiwa na elimu hiyo huku wakibainisha changamotio zao.

Sauti ya wafanyabiashara Pemba.

Kilele cha mwezi wa Kurejesha Shukrani kwa mlipa kodi kwa hapa kisiwani  kinatarajiwa kughitimisha Disemba 28 kwa kutoa zawadi na tunzo mbali mbali kwa walipa kodi.