Zenj FM

CUF Pemba wailaumu ACT Wazalendo kushindwa kuwatetea wananchi

21 August 2023, 2:38 pm

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF wilaya ya Chake Chake Moh`d Haji Kombo akizungumza na wanachama wapya waliojiunga na chama hicho katika kijiji cha Gawani kilichopo jimbo la Ole. Picha na Is-haka Mohammed

Chama cha Cuf Pemba imekitupia lawama chama cha Act Wazalendo kwa kushindwa kuisimamia Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar katika swala zima la upandaji wa bei za bidhaa hasa vyakula.

Na. Is-haka Mohammed Pemba.

Chama cha Wananchi CUF kimetoa lawama kwa chama cha ACT Wazalendo wakidai kushindwa kutetea kuendelea kwa mfumo wa  bei ya chakula hasa mchele na sukari licha ya kuwemo ndani ya serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Lawama hizo za CUF zimeelezwa kwenye shughuli ya upandishaji wa Tawi jipya ya CUF katika kijiji cha Gawani Kilichopo jimbo la Ole Wilaya, Mkoani wa Kusini Pemba na viongozi wa chama hicho wakati wakizungumza na wanachama.

Kaimu Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Chake Chake Rashid Ali Hamad amesema chama hicho ambacho kimetoa Waziri wa Biashara na Viwanda Omar Said Shaaban hakioneshi kuguswa na upandaji wa bei hizo kwa kudai ukimya wa Waziri huyo ni viashiria tosha vya kushindwa kumsaidia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.

Sauti ya Kaimu Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Chake Chake Rashid Ali Hamad

Kwa upande wake Katibu wa CUF Wilaya ya Chake Chake Moh`d Haji Kombo amemuomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi  kuchukua hatua za kukabili hali ya mfumo wa bei ya chakula kwani wanaoathiriki ni wananchi wenye kipato cha chini.

Sauti ya Katibu wa CUF Wilaya ya Chake Chake Moh`d Haji Kombo