Wamiliki wa Mahotel wakumbushwa haki na wajibu wao wilaya ya Kati
14 August 2023, 3:01 pm
Wamiliki wa Mahoteli wilaya ya Kati ametakiwa kuzipitia sheria na Kanunu za Serikali za Mitaa katika huduma ya uzoaji wa taka ili kuepusha migogoro baina yao na Baraza la mji.
Wafanyabiasha wa Mahoteli Wilaya ya Kati wameshauriwa kuzisoma vyema Sheria na Kanuni za huduma ya taka kama zilivyo ainishwa na Serikali ili kufahamu haki na wajibu wao
Mwenyekiti wa Baraza la Mji Kati Said Hassan Shaaban, ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Wadau juu ya huduma ya taka katika Mahoteli ya Wilaya ya Kati, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkoa wa Kusini Unguja Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
Amesema mkutano huo umelenga kuwakumbusha wamiliki wa Mahoteli kuwa Serikali za Mitaa ndizo ambazo zinawajibika katika suala Zima la huduma ya taka wanazo zizalisha hivyo nivyema kuzipitia ipasavyo sheria na Kanunu ambazo zinaongoza utekelezaji huo ili kuondokana na changamoto zinazojitokeza miongoni mwao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Mji Kati Salum Mohamed Abubakar amesema lengo la kutoa elimu kwa wamiliki wa mahoteli ni kukumbushana juu ya taratibu na sheria zinazo waongoza katika ukusanyaji wa taka na utunzaji wa mazingira.