Wajasiriamali zanzibar watakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora
30 November 2021, 12:55 pm
Na Mary Julius: Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, amewataka wajasiri amali hasa vijana kuzalisha bidhaa zenye ubora zinazoweza kuhimili ushindani wa soko la biashara nchini.
Othman ameyasema hayo alipozungumza katika hafla ya kukabidhi ruzuku za fedha kwa vikundi 15 vya vijana wajasiriamali kutoka Bara na Zanzibar huko katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizi zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la Marekani la USAID
Othman amewakumbusha vijana kuhakikisha fedha walizopewa zinatumika ipasavyo kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuwawezesha vijana kuzalisha bidhaa mbali mbali kupitia vikundi vyao kwa nia ya kujikwamua kiuchumi.
Aidha amesema fedha hizo dola milioni moja zilizotolewa kwa vikundi hivyo kupitia Mradi wa Inua Vijana, iwapo zitatumika ipasavyo na kwa malengo yaliyokusudiwa zitaweza kutoa matokeo mazuri ya kimaendeleo kwa vijana nchini.