Wasafirishaji wa watalii forodhani kwenda visiwani walia na tozo ya chabanca
22 November 2021, 2:17 pm
Na Mary Julius na Thuwaiba Mohd: Jumuiya ya wavuvi na wasafirishaji wa watalii forodhani mchanga wameiomba serikali kuangalia upya suala la chabanca kuhusu kuweka meza ya kutoza kodi katika eneo la forodhani.
Kauli hizo imefuatia baada ya kampuni ya chabanca kwenda katika eneo hilo kuweka meza kwa ajili ya kuwatoza tozo watalii wanao kwenda visiwani bila ya jumuiya hiyo kuishirikisha.
Wakizungumza na zenj fm baadhi ya wanajumuiya hiyo wamesema ni vyema serikali inapoamuwa jambo ikawashirikisha wahusika ili nawao wakatowa mawazo yao hasa katika kuhakisha sekta ya utalii inakuwa zanzibar.
Akitolea ufafanuzi juu ya suala hilo mwenyekiti wa kamati tendaji ya wavuvi na hifadhi ya mjini chabanka Iddi Omar Khamis amesema chabanca itakaa na jumuiya hiyo ili kuzungumza nao juu ya tozo hizo na kuhakikisha wanaendana na kasi ya maendeleo ya uchumi wa bluu hasa katika sekta ya utalii .