Keifo FM

Serikali na wadau mguu sawa elimu ya Ukimwi Kyela

25 November 2024, 15:14

Mratibu wa Ukimwi wilaya ya Kyela Amosi Kayembele aikiwa na timu ya watalamu kutoka hospitali ya wilaya ya kyela pamoja wadau kutoka shirika lisilo la kiserikali la Tumaini wakiwa katika kipindi cha Morning Power Picha na Masoud Maulid

Kuelekea maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yanafanyika Desemba 1 kila mwaka serikali ya halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa kushirikiana na wadau wamejipanga kutoa elimu ya ukimwi kwa wananchi wilayani hapa.

Na Masoud Maulid

Halmashauri ya wilaya ya kyela kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamedhamiria kuadhimisha siku ya ukimwi duniani kwa vitendo zaidi na kutoa taarifa ya utekelezaji kwa kila asasi na wadau.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa kudhibiti ukimwi wilaya ya kyela Amosi Kayembele katika kipindi cha morning power akielezea mikakati iliyopangwa katika kuelekea maadhimisho hayo ambapo amesema mwaka huu wadau na asasi wamelenga kuzifikia kata kumi na tatu kutoa elimu kwa vitendo  ili kuleta ufanisi mzuri.

sauti ya Kayembele

Kayembele ameongeza kuwa  kata kumi na tatu zitakazofikiwa na wadau pamoja na  asasi katika kipindi cha kuelekea kuadhimisha siku ya ukimwi duniani zitapatiwa elimu ya hamasa juu ya ukimwi ili jamii iweze kushiriki kwenye mapambano dhidi ya ukimwi,kuhamasisha upimaji,elimu ya tohara na elimu kupinga ukatili wa kijinsia.

Amosi Kayembele

Kwa upande wa daktari Saimoni Mduma maratibu wa kudhibiti ukimwi afya amesema malengo ya kitaifa na kimataifa ya kudhibiti ukimwi ni ifikapo 2030 kusiwe na maambukizi mapya ya ukimwi ambapo kwa hali ya maambukizi kwa wilaya ya kyela kwa kuanzia januari hadi septemba mwaka huu,waliojitokeza kupima ni 39062 majibu hasi ni 37816 na majibu chanya ni 1246 sawa na asilimia 3.1.

sauti ya Daktari wilaya ya Kyela

Katika hatua nyingine daktari kutoka hospitali ya wiaya ya kyela amesema moja ya njia inayoweza kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa mwanaume ni  kufanyiwa tohara ambayo huzuia maambukizi kwa asilimia sitini hivyo ameitaka jamii kujitokeza kwa kuwa zoezi ni bure,

Sauti ya Mganga

Katika kuhakikisha jamii inapata elimu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi shirika la tumaini limekuwa na mradi unaolenga kutoa elimu kwa wasichana kuanzia umri wa miaka kumi na tano hadi ishirini na nne kwa kuwafikia kwenye jamii zao ili waweze kupima na kujua hali zao za maambukizi japo kumekuwa na changamoto kadhaa hasa kutoka kwa baadhi ya wazazi.

sauti mtaalamu ktoka shirika la tumani

Maadhimisho ya siku ya ukimwi dunia hufanyika kia mwaka desemba mosi na kauli mbiu ya mwaka huu ni chagua njia sahihi tokomeza ukimwi.