Keifo FM

Wizara ya Ardhi yatinga Kyela na mkakati maluum

20 June 2024, 21:21

Mgeni rasmi wa mkutano wake wa kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase akiwa ameambatana na katibu tawara wilaya ya Kyela Picha na James Mwakyembe

Wananchi wilayani watametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la urasimishaji wa ardhi pamoja na kumiliki hati za umilikaji wa ardhi zoezi litakaloendeshwa na wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi baadae mwaka huu.

Na James Mwakyembe

Wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo imefanya mkutano wake na wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi hapa wilayani Kyela mgeni rasmi akiwa mkuu wa wilaya Josephine Manase.

Mradi huu unatarajiwa kuwa mwarobaini wa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiwakumba wakazi wengi wilayani hapa kutokana na kutojua umuhimu wa kurasimisha ardhi pamoja na kuwa na hati milki hali ambayo imekuwa ikiwatumbukiza katika migogoro isiyo ya lazma.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Songwe View Resort kata ya Ikimba hapa wilayani kyela mkuu wa wilaya ya kyela Josephine Manase amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassani kwa kuipa kipaumbele wilaya ya kyela kuwa miongoni mwa wanufaika wa maradi huo ambao unakuja kuinua hadhi ya wilaya kwa ujumla.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya kyela kuhusu pongezi kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania 11

Ameongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na kasi kubwa ya ukuuaji wa miji na vijiji kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu hali inayosababisha uhitaji wa ardhi kuwa mkubwa miongoni mwa wananchi hivyo mradi huu unakuja katika muda muafaka ambapo jumla ya vijiji tisini vitafikiwa na mradi huu mjini na vijijini

Sauti ya mkuu wa wilaya kuhusu kasi ya ukuuji wa miji na vijiji 22

Amesema mradi huo umelenga kusimika mfumo uunganishi wa kietroniki wa kuhifadhi kumbukumbu za ardhi katika ofisi zote za ardhi za mkoa na halmashauri mbalimbali hapa nchini kwa kuzingatia sera ya utandawazi ili kuendana na kasi ya maendeleo ya dunia yanayohusiana na makubaliano ya kiuchumi yanaiyoitaka Afrika kuhakikisha upangaji bora na umiliki wa ardhi mijini na vijijini

Sauti mkuu wa wilaya kuhusu mfumo wa kietroniki33
Pichani wadau mbalimbali waliojitokeza katika ukumbi wa Songwe View Resort katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi hapa wilayani kyela

Awali akitoa neno la utangulizi kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kyela Saumu Kumbisaga amemshukuru Rais wa jamahuri ya muungano wa Tanzania pamoja na wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kwa kuuleta mradi huo kyela na kusema serikali imeupokea.

Kwa upande wake Tumaini Setumbi ambaye ni afisa maendeleo ya jamii mwandamizi kutoka wizara ya ardhi makao makuu Dodoma amesema wakati wizara ikiandaa nyaraka mbalimbali za kuhakikisha wanapata fedha walitumia miongozo mbalimbali ya kisheria za nymbani na kimataifa lengo likiwa ni kulinda kuishirikisha jamii husika.

Sauti ya Tumaini Setumbi kuhusu uandaaji wa nyraka za kupata fedha za mradi

Mradi huo unatarajiwa kufika katika mitaa ya  Ipinda,Mikumi,Itunge,Bondeni A,Bondeni B,Serengeti,na Ndandalo,ambapo kabla ya kuanza utekelezaji wizara inatarajia kuhamasisha wananchi juu ya uelewa wa mradi huo.