Keifo FM
Keifo FM
12/03/2026, 13:05

Wananchi wa ubalozi wa Msasani kitongoji cha Ipyana wilayani kyela wamehamasishana kulima barabara korofi kipindi hiki cha Mvua za masika na kupelekea kukosekana kwa mawasiliano kati ya ubalozi wao na balozi zingine.
Na Masud Maulid
Wananchi wa ubalozi wa msasani kitongoji cha ipyana a kata ya ipyana wilaya ya kyela wamejitokeza kushiriki zoezi la kujitolea kulima barabara iliyopo kwenye ubalozi huo kwa lengo la kurahisisha mawasiliano pamoja na kuepukana na maji kujaa kwenye makazi yao.
Akizungumza na mwandishi wa habari balozi wa eneo hilo Widley Mwasyika amaesema uamuzi wa wananchi kujitolea kufanya kazi hiyo ni kutokana na changamoto ya ubovu wa barabara kutopitika wakati wa masika na kupelekea maji kujaa kwenye makazi yao.
Mwasyika ameongeza kuwa matengenezo hayo yatasaidia wenye viwanja pia kuuza kwa bei nzuri kutokana na miundombinu kupitika,kurahisisha usafirishaji mazao kutoka mashabani pamoja na wananchi kwenda kupata huduma za kijamii nje ya ubalozi wao.
Baadhi ya Wananchi wanaoshiriki zoezi hilo wamesema, moja ya sababu inayowahamasisha kushiriki kulima barabara ni kutokana na maeneo ya ubalozi kupata shida kipindi cha masika maji kukosa mwelekeo na kujaa kwenye makazi yao,huku Bernadi Nindi akiongeza kuwa,eneo hilo limekuwa changamoto pia kwa watu wenye vyombo vya moto kuvipaki mbali na makazi yao.
Eneo la Ubalozi wa Msasani kata ya Ipyana Wilaya ya Kyela awali lilitumika kwa shughuli za kilimo kabla ya kuanza kujenga nyumba na sasa kuwa eneo la makazi.
