Keifo FM
Keifo FM
5 February 2026, 14:08

kijana mwenye umri wa miaka 30 wilayani kyela anaye fahamika kwa jina la Mogela Odian Kipeta amehukumiwa kwenda jela kwa kujinufaisha kingono na mtoto mwenye umri wa miaka 8.
na Emmanuel Jotham
Mahakama ya Wilaya ya Kyela imemuhukumu Mogela Odian Kipeta, (30) Mkazi wa Kasumulu, Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kujinufaisha kingono alilolitenda dhidi ya mtoto mwenye umri wa miaka 08 ambaye ni Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kasumulu.
Hukumu hiyo imetolewa Februari 3, 2026 na Mhe.Hakimu Paul Barnabas (SRM) ambapo Akisoma hukumu hiyo Mheshimiwa Hakimu Barnabas alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 138B kifungu kidogo cha kwanza (f) cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2023.
Mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 25, 2025 baada ya kumkuta mhanga akiwa anacheza na Wanafunzi wenzake maeneo ya jirani na Shule yao muda wa mapumziko ya vipindi vya masomo ndipo alimlaghai kwa pipi na biscuit na alipomfikisha nyumbani kwake alimvua nguo zote na kumfanyia vitendo vya kingono kwa ajili ya kujinufaisha kingono.
Mwendesha mashitaka wa Serikali Wakili Davice Msanga (SA) akiwa mahakamani hapo alimuomba Mhe.Hakimu kutoa adhabu kali