Keifo FM

Mhandisi Kasekenya aanza kampeni za ubunge Ileje

10 September 2025, 16:03

Pichani ni mgeni rasmi na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Songwe Ndg Mwampashi Selembe Mwanamvuliwankondo Na James Mwakyembe

“Ukichagua CCM umechagua afya bora,barabara nzuri,maji salama,elimu na umeme vijijini”

Na James Mwakyembe

Mamia ya wananchi wamejitokeza katika uzinduzi wa kamapeni za kumnadi mgombea wa ubunge kupitia chama cha Mapinduzi CCM jimbo la Ileje mkoani Songwe Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya zikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Mwampashi Selembe Mwanamvuliwankondo.
Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya kijiji cha Mtula kata ya Lubanda halmashauri ya wilaya ya Ileje ikihudhuliwa na wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya wilaya pamoja na Mkoa wa Songwe.
Akizungumza wakati wa kumnadi mgombea wa ubunge jimbo hilo Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya Mwampashi amesema kutokana na kazi kubwa zilizofanywa na mgombea huyo katika miaka mitano iliyopita zinatosha kusimama tena mbele ya wananchi na kuomba ridhaa nyingine ya kuliongoza jimbo hilo.

Sauti ya Mgeni rasmi 11

Kwa upande wake Mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Ileje Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya amewaambia wananchi wote waliojitokeza katika kampeni hizo sababu za kwanini wakichague chama hicho huku akiinadi Ilani ya chama jinsi kilivyotekeleza miradi mingi katika kipindi chake cha miaka mitano iliyopita.

Sauti ya Mhandisi Kasekenya kuhusu yaliyofanyika 22
Picha ya wananchi wa Ileje waliojitokeza katika uzinduzi wa kumnadi mgombea wa ubunge na madiwani katika jimbo la hilo.

Kuhusu yapi yanayoatarajiwa kufanyika katika kipindi kijacho cha miaka mitano ijayo Mhandisi Kasekenya amesema.

Sauti ya Mhandisi Kasekenya 33

Akizungumza kwa niaba ya Machifu wa Ileje Chifu Mwampashi amesema

Sauti ya mwakilishi wa machifu