Keifo FM
Keifo FM
10 June 2025, 18:06

“Nilipata mashaka kupitisha makato ya shilingi hamsini kwa kila kilo nikihofia kuwa je zitaleta faida?”
Na Nsangatii Mwakipesile
Mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Homera ameshiriki zoezi la kukabidhi vipima unyevu wa Kakao kwa AMCOS 37 hapa wilayani kyela katika zoezi lililohudhuliwa na mbunge wa jimbo la Kyela Ali Mlaghila Kinanasi.
Vipima unyevu hivyo vinatolewa kwa lengo la kuwasaidia wakululima wa zao la Kakao kuuza zao hilo likiwa katika viwango stahiki tofauti na hapo awali ambapo wakulima wengi walilazimika kuuza bila kupimwa hali ilipelekea kupoteza mapato mengi.
akikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni mizani arobaini na vipima unyevu kwa AMCOS hizo 37 mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amewagiza wanufaika wote kuzitunza mizanai hizo pamoja na kuhakikisha kila chama msingi kuwa na vitaru kwajili ya kugawa kwa wakulima.
Akitoa tarifa kwa mgeni rasmi wa zoezi hilo lililofanyika katika ofisi Ghala kuu Kyecu ltd Kyela mjini Kaimu Meneja wa kyecu Nabii Emmanuel amesema zaidi ya shilingi milioni mia tano zimetumika kununua vifaa hivyo fedha iliyotokana na makato ya shilingi hamsini kwa mkulima kwa kila kilo itakayouzwa ghalani hapo.

Naye Mbunge wa jimbo la kyela Ally Mlaghila amemaliza kwa kuwapongeza wakulima wa zao la kokoa na chama cha msingi kyecu huku akiwahimiza kuhakikisha wanauza Kakao iliyo na ubora ili kukidhi soko la kimataifa.

Wilaya ya Kyela ni moja kati ya wilaya chache hapa nchini tanzania yanayozarisha Kakao yenye ubora mkubwa duniani hivyo serikali imeamua kuwekeza nguvu kwa wakulima wa zao hilo kuhakikisha kakao inayouzwa inakidhi viwango vya kimataifa.