

20 February 2025, 16:55
Katika hali ya kushangaza serikali ya halmashauri ya wilaya ya kyela imeagiza mkaguzi wa hesabu za serikali kufika katika kijiji cha kafundo kutokana na harufu ya ubadhilifu wa fedha za wananchi.
Na Masoud Maulid
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Katule Godfrey Kingamkono amemuagiza Mkaguzi wa ndani kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha ziadi ya milioni tatu zinazolalamikiwa na wananchi wa kijiji cha Kafundo kutokujua matumizi yake.
Kauli hiyo ameitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha kafundo baada ya kumlalamikia Afisa Mtendaji wa kijiji Venance Mwangalaba kutosoma mapato na matumizi kwa muda wa miaka mitatu hali ambayo imepelekea maswali mengi kwa wananchi kijijini hapo.
Katika mkutano huo ambao wananchi wameibuwa hoja zinazohitaji majibu kutoka kwa Afisa Mtendaji ikiwemo kutokupata taarifa ya fedha zilizochangwa kwa ajili ya kulima barabara zaidi ya shilingi laki nane,fedha zaidi ya milioni mbili kutoka ofisi ya Mbunge kwa ajili ya ujenzi wa karavati pamoja na fedha zinazotokanana kukodisha mashamba ya kijiji.
Mtendahi wa kijiji cha kafundo Venance Mwangalaba baada ya kuhojiwa kwenye mkutano huo amekanusha taarifa za wananchi kutosomewa mapato na matumizi kwa muda wa miaka mitatu na kubainisha kuwa amekuwa akisoma mapato na matumizi na amelazimika kuonesha mihtasari ambayo imebainika kuwa na kasoro kadhaa.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu Mwenyekiti wa Halmashauri amelazimika kumwagiza mkaguzi wa ndani kupitia na kukagua taarifa zote za fedha kwa miaka mitatu na majibu ya uchunguzi huo kutolewa siku ya jumanne ya february 25 mwaka huu kwenye mkutano wa kijiji.
Kafundo ni miongoni mwa Vijiji kumi na moja vinavyounda kata ya Ipinda na inavyanzo vya mapato ikiwemo mashamba 102 pamoja na machinjio ya ngo’mbe.