

12 February 2025, 17:37
Katika kutekeleza agizo la serikali la kutoa mikopo ya asilimia kumi kutokana na makusanyo ya ndani,halmashauri ya wilaya ya Kyela imeanza kutekeleza agizo hilo kwa kutoa mikopo ya shilingi milioni 816 kwa vikundi 65 kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
Na Masoud Maulid
Jumla ya shilingi milioni mia nane kumi na tisa zimetolewa na halmashauri ya wilaya ya kyela na kukopeshwa kwa vikundi sitini na tano vya wajasilia mali mgeni rasmi akiwa mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase.
Hafla hiyo ya utoaji mikopo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya kyela ambapo vikundi mbalimbali vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliokidhi vigezo wamepatiwa mikopo hiyo ambayo imekuwa ikitolewa na serikali kutokana na mapato ya ndani.
Akikabidhi hundi ya mfano mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya kyela Josephine Manase ameishukuru serikali kwa kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa makundi ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu huku akisema mikopo hiyo itasaida kuwakwamua kiuchumi.
Mkuu wa wilaya ameongeza kuwa baada ya serikali kutoa mikopo hiyo wanafaika wanapaswa kuitumia vizuri kwa kufanya shughuli zilizolengwa wakati wa kuomba mikopo ili kupata urahisi wa kurejesha ikiwa ni Pamoja na kufanya shughuli za maendeleo.
Katika taarifa iliyosomwa na Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya kyela Victor Kabuje amesema fedha zilizotengwa kutoka ofisi ya mkurugenzi ni kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia tisa tisini na moja ambapo mchakato wa kutoa mikopo umefanyika na kuhakiki uwepo wa vikundi na hadi sasa kwa wilaya ya kyela hakuna vikundi hewa
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la kyela Ally Mlaghila amempongoza Mkuu wa Wilaya pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuratibu na kusimamia vizuri mchakato wa kuvipata vikundi huku akimpongeza Afisa maendeleo ya jamii kwa kutoa ufafanuzi pale yalipotokea malalamiko ya baadhi ya vikundi kukosa mkopo.
Mikopo ya Halmsahuri ya asilimia kumi yenye lengo la kuwakwamua kiuchumi makundi ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu imetangazwa kurejeshwa novemba 30 mwaka jana baada ya kusitishwa na Serikali ili kujiridhisha upya kwa wanufaika wa mikopo hiyo.