Keifo FM

Kyela:Wiki ya sheria kyela kumekucha

28 January 2025, 14:48

Pichani ni hakimu mkazi mkuu mfawidhi wilaya ya Kyela Andrew Severin Njau

Wananchi wilayani kyela wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya kyela kwenda kutoa na kero zao ili zitatuliwe katika wiki hii ya sheria.

Na James Mwakyembe

Hatiamaye maadhimisho ya wiki ya sheria yamezinduliwa rasmi hapa wilayani kyela huku wananchi wakitakiwa kujitokeza kwa wingi katika kilele cha siku hiyo kitakachofanyika februari 3 mwaka huu katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya kyela.

Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaongozwa na dira inayosema Tanzania ya mwaka 2050 nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo ambapo mahakama wilayani hapa imejipanga kutoa elimu kwa wananchi katika Nyanja mbalimbali pamoja na kutoa miasaada ya kisheria.

Akizungumza na mwandishi habari wa keifo fm hakimu mkazi mkuu mfawidhi wilaya ya Kyela Andrew Severin Njau amewataka wananchi wilayani hapa kujitokeza kwa wingi katika kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika siku ya jumatatu februari 2 katika viunga vya mahakama ya wilaya ya Kyela huku mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa wilaya ya kyela Josephine Manase.

Sauti ya Njau kuhusu wananchi kufika kwa wingi 1
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Itunge hapa wilayani kyela wakipatiwa elimu katika wiki ya sheria

Amesema kuelekea kilele hicho mahakama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamejipanga kutoa elimu kuhusu msaada wa kisheria katika Nyanja za migogoro ya ardhi,mirathi,ukatili wa kijinsia pamoja sheria za madai kwa jamii,hivyo kutoa shime kwa wanachi kujitokeza kwa wingi na kuacha kuogopa makama kama sehemu hatarishi kwao.

Saut ya Njau kuhusu elimu itakayotolewa kwa jamii 2
Baadhi ya walimu katika shule msingi Itunge wilayani kyela wakipatiwa elimu ya masuala yahusuyo haki za kisheria kutoka kwa watalamu wa sheria katika wiki hii ya maadhimisho ya wiki ya sheria yanayoendelea

Kuhusu mashauri yaliyoshika kasimkubwa kwa mwaka wa mahakama uliopita amesema mashauri ya kingongono ndiyo yaliyoripotiwa sana hali iliyopelekea baadhi ya wananchi kuathirika kwa watoto wao kukatishwa ndoto za kielimu.

Sauti ya Njau kuhusu matukio yaliyolipotiwa zaidi mwaka uliopita 3

Kufanyika kwa maadhimisho ya wiki ya sheria huashiria kufunguliwa rasmi kwa mwaka wa mahakama hapa nchini Tanzania ambapo mhimili huo muhimu hutumia muda huo kutoa elimu ya kisheria kwa wanachi ili kuzijua haki zao za msingi zihusuzo haki sheria.